Pata taarifa kuu
SRI LANKA-USALAMA-UCHUNGUZI

Sri Lanka: Mashambulizi dhidi ya makanisa na hoteli ni ulipizaji kisasi kwa mauaji ya Christchurch

Mashambulizi ya Jumapili ya Pasaka nchini Sri Lanka yalitekelezwa kwa kulipiza kisasi mauaji yaliyotokea mwezi uliopita katika Misikiti ya Christchurch, nchini New Zealand, Waziri wa Ulinzi wa Sri Lanka amesema.

Wanawake wawili wkiomboleza waathirika wa mlipuko wa bomu kwenye Kanisa la St Sebastian huko Negombo Aprili 23, 2019, siku mbili baada ya mashambulizi ya Sri Lanka siku ya Pasaka
Wanawake wawili wkiomboleza waathirika wa mlipuko wa bomu kwenye Kanisa la St Sebastian huko Negombo Aprili 23, 2019, siku mbili baada ya mashambulizi ya Sri Lanka siku ya Pasaka Jewel SAMAD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Sri Lanka, Ruwan Wijewardene, amebaini kwamba makundi mawili ya Kiislamu kutoka Sri Lanka, ikiwa ni pamoja na National Thawheed Jama'ut (NTJ), walihusika pengine katika mfululizo wa mashambulizi yaliyolenga makanisa na hoteli, na kusababisha vifo vya watu 321, ikiwa ni pamoja na raia wa kigeni 38, kwa mujibu wa taarifa ya mwisho iliyotolewa leo Jumanne.

"Ripoti za kwanza za uchunguzi zinaonyesha kuwa mashambulizi dhidi ya makanisa na hoteli nchini Sri LAnka yalitekelezwa kwa kulipiza kisasi mashambulizi dhidi ya misikiti miwili, yaliyosababisha vifo vya watu wengi nchini New Zealand," Waziri wa Ulinzi wa Sri Lanka, ameliambia bunge.

Mwezi uliopita, raia mmoja wa Australia mwenye umri wa miaka 28, Brenton Harrison Tarrant, aliua waumini 50 kwa kuwapiga risasi katika misikiti miwili ya mji wa Christchurch nchini New Zealand, na kurusha mauaji hayo moja kwa moja kwenye mtandao wa Facebook.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.