Pata taarifa kuu
UKRAINE-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais Ukraine: Mshekeshaji Volodymyr Zelenskiy aibuka mshindi

Mchekeshaji na ambaye hakuwa maarufu katika siasa nchini, Volodymyr Zelenskiy, amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais nchini Ukraine uliofanyika Jumapili (Aprili 21) dhidi ya rais anaye maliza muda wake Petro Poroshenko.

Volodymyr Zelenskiy baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais, akisherehekea na wafuasi wake, Aprili 21, 2019 Kiev.
Volodymyr Zelenskiy baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais, akisherehekea na wafuasi wake, Aprili 21, 2019 Kiev. REUTERS/Valentyn Ogirenko
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wake wameendelea kusherehekea ushindi wa kiongozi wao usiku kucha katika ngome yao kuu ya kampeni wakati wa uchaguzi huo wa urais, kwa mujibu wa mwandishi wetu, aliyetumwa Kiev, Anastasia Becchio.

Volodymyr Zelenskiy ameshinda kwa 73% ya kura na kumuangusha rais anaye maliza muda wake Petro Poroshenko.

Rais Poroshenko amekubali kushindwa na kumpongeza rais mteule kwa ushindi wake.

Bwana Zelensky mwenye umri wa miaka 41, amewaambia wafuasi wake "sijawa rais bado, lakini kama raia wa Ukraine, ninaweza kuwaambia nchi zote za Kisovieti kuwa watuangalie sisi, kila kitu kinawezekana !"

Zelensky anajulikana kwa umahiri wa ucheshi wake kama muigizaji nyota wa mfululizo wa filamu ya satirical kwenye televisheni ambapo anaigiza kama rais wa Ukraine.

Zelensky amekuwa akicheza mchezo wa kuigiza unaoitwa 'Servant of the People ' ambapo kwa bahati tu akawa muigizaji anayetaka kuwa rais wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.