Pata taarifa kuu
JPANI-SIASA-JAMII

Mfalme mpya wa Japan kukabidhiwa mamlaka mwezi ujao

Japan imetangaza kuwa Mfalme mpya Prince Naruhito, mwanawe Akihito, ataanza kazi mwezi ujao. Prince Naruhito atachukua nafasi ya babake, Mfalme Akihito mwenye umri wa miaka 85, ambaye mwaka 2016 aliomba kustaafu.

Mwanamfalme Naruhito (kushoto) na baba yake Akihito (kulia) wakati wakitoa salamu za Mwaka Mpya.
Mwanamfalme Naruhito (kushoto) na baba yake Akihito (kulia) wakati wakitoa salamu za Mwaka Mpya. Kazuhiro NOGI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwaka 2016 Mfalme Akihito, mwenye umri wa miaka 83, alielezea azma yake ya kuachia mamlaka kwa sababu za kiafya.

Baraza la Mawaziri liliunga mkono mpango huo, ambao sasa ulipelekwa bungeni na kuweza kuidhinishwa.

Mfalme mpya wa Japan, atafahamika kwa jina la Reiwa, jina linalomaanisha amani na utengamano.

Mfalme Akihito mara kwa mara ameeleza masikitiko yake kutokana na vitendo vya Japan wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, jambo lililomfanya kutofautiana na viongozi kadha waliotaka kubadilisha mwenendo wa taifa hilo.

Mwaka 2011, Mfalme Akihito na Malkia Michiko walisifiwa kwa kutembelea maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga na tetemeko la ardhi. Mfalme Akihito pia alitoa hotuba yake ya kwanza kwa umma kupitia video.

Mfalme Akihito amekuwa utawalani tangu mwaka 1989.

Akihito ndiye Mfalme wa 125 katika familia ya kifalme ambayo inaaminika kutawala tangu karne ya tano, jambo linaloifanya kuwa familia ya kifalme ya kale zaidi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.