Pata taarifa kuu
IRAN-MAJANGA YA ASILI

Mafuriko yaua kumi na nane Iran

Watu wasio pungua 18 wamefariki dunia na 68 wamejeruhiwa nchini Iran kufuatia mafuriko yanayoendelea katika mikoa kadhaa, idara ya huduma za dharura nchini Iran imesema Jumatatu wiki hii.

Picha iliyotumwa tarehe 25 Machi 2018 na Shirika la Habari la Mehr, likionyesha magari yaliopinduka wakati wa mafuriko katika mji wa Shiraz kusini mwa Iran.
Picha iliyotumwa tarehe 25 Machi 2018 na Shirika la Habari la Mehr, likionyesha magari yaliopinduka wakati wa mafuriko katika mji wa Shiraz kusini mwa Iran. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Takwimu hii mpya ya vifo 18 imetolewa na idara ya huduma za dharura kwenye tovuti yao. Hapo awali, mmoja wa viongozi wao, Pirhossein Koolivand, aliiambia runinga ya serikali kuwa watu wasio pungua 11 wamefariki na 68 wamejeruhiwa katika mji pekee wa Shiraz, kusini mwa Iran, na mwingine amefariki dunia katiika mji wa Sar- e Pol-e Zahab, katika mkoa wa Kermanshah, magharibi mwa Iran.

Iran inakabiliwa na mafuriko ambayo hayajawahi kutokea katika taifa hilo katika mikoa 25 kati ya 31, kwa mujibu wa idara ya Udhibiti wa majanga ya asili.

Mafuriko hayo yametokea hasa magharibi na kusini magharibi mwa nchi, siku kadhaa baada ya mafuriko ya Machi 19 katika majimbo ya Golestan na Mazandaran, kaskazini mashariki mwa nchi. Hakuna ripoti rasmi ya uharibifu katika mikoa hiyo iliyotolewa.

Shughuli za idara ya huduma za dharura zinapungua kwa kutokuwepo kwa wafanyakazi wengi ambao wako likizo, wakati Iran inadhimisha Mwaka Mpya wa Kiajemi.

Idara ya Udhibiti wa majanga ya asili na Wizara ya Afya, yenye dhamana ya hospitali, wamefuta likizo zote na wametaka wafanyakazi kurudi kazini haraka iwezekanavyo . Wakuu wa mikoa wamepewa agizo la kusalia kazini.

Mvua zitaendelea kunyesha hadi Jumatano, mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini Iran imeonya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.