Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Mauaji ya Kim Jong-nam: Mtuhumiwa aachiwa huru

media Siti Aisyah alikuwa anashtumiwa sawa na Doan Thi Huong, raia wa Vietnam mwenye umri wa miaka 30, kuwa alimwagia usoni Kim Jong-nam tindikali aina ya VX, ambayo ni sumu kali, Februari 13, 2017 katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia. REUTERS/Lai Seng Sin

Mahakama ya Malaysia imeiachana na kesi dhidi ya raia wa Indonesia anayeshtumiwa kuhusika katika mauaji ya Kim Jong-nam, kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, aliyeuwana mnamo mwaka 2017.

Siti Aisyah, mwenye umri wa miaka 26, ameachiwa huru na ataweza kurudi nyumbani, amesema mwendesha mashitaka mkuu.

Siti Aisyah alikuwa anashtumiwa sawa na Doan Thi Huong, raia wa Vietnam mwenye umri wa miaka 30, kuwa alimwagia usoni Kim Jong-nam tindikali aina ya VX, ambayo ni sumu kali, Februari 13, 2017 katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia.

Leo Jumatatu waendesha mashitaka wametoa taarifa mbele ya mahakama kuwa wamepewa maagizo ya kuachana na mashitaka ya mauaji dhidi ya Siti Aisyah, bila kutoa maelezo zaidi.

Katika barua ya tarehe 8 Machi mwaka huu, iliyotumwa kwa Waziri wa Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Malaysia Tommy Thomas, alibaini kwamba amefanya hivyo kufuatia ombi viongozi wa serikali nchini Indonesia.

Ingawa mashtaka ya mauaji yamefutwa, mahakama imefutilia mbali ombi la wanasheria wake wa kufutiwa mashitaka yote yanayomkabili."Sisi bado

Tunaamini kwamba mteja wetu alitaka kutolewa tu kama kafara," mmoja wa wakili wa Siti Aisyah, Gooi Mara Seng, ameviambia vyombo vya habari, huku akiongeza "bado nadhani Korea Kaskazini inahusika na hilo."

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana