Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Kim Jong-un awasili Hanoi kwa mkutano wake na Trump

media Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amewasili Hanoi ambako atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump Jumatano na Alhamisi kwa mkutano wa pili ambapowawili hao watajaribu kukubaliana juu ya ahadi za Pyongyang kuachana na mpango wake wa kutengeneza sila REUTERS/Ann Wang

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amewasili katika mji mkuu wa Vietnam, Hanoi, mapema Jumanne asubuhi, ambako atakutana na rais wa Marekani Donald Trump Jumatano na Alhamisi wiki hii.

Mkutano huu utakuwa wa pili ambapo wawili hao watajaribu kukubaliana juu ya ahadi za Pyongyang kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia.

Donald Trump, ambaye aliondoka Marekani Jumatatu mchana wiki hii anatarajiwa kuwasili jijini Hanoi leo Jumanne usiku.

Akizungumza akiwa katika ndege ya rais ya Air Force One, msemaji wa White House, Sarah Sanders, amesema kuwa Trump na Kim watakutana ana kwa ana Jumatano jioni, kabla ya chakula cha jioni.

Sarah Sanders amesema kuwa vikao vipya kati ya viongozi hao wawili vimepangwa kufanyika siku ya Alhamisi.

Katika mkutano wao wa kwanza wa kihistoria mnamo mwezi Juni mwaka jana huko Singapore, Trump na Kim waliahidi kufanya kazi ya kwa pamoja kwa lengo la kuachana moja kwa moja na mpango wa silaha za nyuklia katika rais ya Korea, lakini hatua chache zimepigwa katika mchakato huo tangu tarehe hiyo.

Washington kwa miaka mingi imekuwa ikiomba Korea Kaskazini kuachana moja kwa moja na mpango wa silaha za nyuklia, kabla ya jambo lolote.

Kim Jong-un, ambaye amewasili kwa treni katika kituo cha mji wa Dong Dang baada ya kuvuka mpaka kati ya China na Vietnam. Ameongozana katika safari hiyo na dada yake na mshauri, Kim Yo-jong.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana