Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuzuru Urusi Jumatano

media Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao Kremlin, Moscow tarehe 10 Machi 2017. Sergei Ilnitsky / POOL / AFP

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, anatarajia kuanza ziara ya kikazi nchini Urusi Jumatano wiki hii. Ziara hii inakuja siku chache baada ya Marekani kutangaza kuwa itawaondoa askari wake nchini Syria. Ushirikiano kati ya Uturuki na Urusi unaendelea kuimarika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya ofisi ya rais, Rais Erdoğan atafanya ziara ya siku moja siku ya Jumatano nchini Urusi na katika ziara hiyo atakutana na rais wa Urusi Vladmir Putin.

Moja kati ya mambo yatakayojiri katika ziara hiyo ni pamoja na mkutano utaofanyika jijini Moscow baina ya wajumbe na mawaziri wa pande hizo mbili. Katika mkutano huo mambo mbalimbali ikiwemo hali ya Syria na mahusiano baina ya mataifa hayo mawili yanatarajiwa kuwa ajenda kuu za mkutano huo.

Uturuki ni mshirika wa mkuu wa Urusi na nchi hizi mbili zinaendelea kushirikiana katika vita nchini Syria dhidi ya kundi la Islamic State.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana