Pata taarifa kuu
JAPAN-GHOSN-UCHUMI-HAKI

Carlos Ghosn akanusha tuhuma dhidi yake

Kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mnamo Novemba 19, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya kutengeneza magari Renault Carlos Ghosn amefikishwa mahakamani akiwa amefungwa pingu mjini Tokyo, nchini Japan.

Mahakama ya Tokyo ambapo Carlos Ghosn amefikishwa Jumanne Januari 8, 2019.
Mahakama ya Tokyo ambapo Carlos Ghosn amefikishwa Jumanne Januari 8, 2019. Kiyoshi Ota/Pool via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Carlos Ghosn, mwenye umri wa miaka 64 amehojiwa leo Jumanne asubuhi na mahakama yaTokyo, baada ya yeye kuomba ahojiwe ili kuweka wazi ukweli kuhusu mashtaka dhidi yake. Wanasheria wake walikuwa wameomba kuwa sababu za kufungwa kwake ziekwe wazi.

"Nilishtumiwa na kufungwa kwa madai yasiyo na msingi," amesema katika taarifa iliyoandikwa aliweza kusoma mbele ya mahakama.

Pia ameeleza kwamba alichukua hatua kwa idhini ya wadau wa kampuni ya kutengeneza magari ya Nissan kutoka Japani: "Nilichukua hatua kwa heshima, kisheria na kwa ujuzi na kwa idhini ya viongozi wa kampuni".

Jaji wa mahakama pia amesema kuwa Carlos Ghosn aliwekwa kizuizini kwa sababu ya hatari ya kutoroka.

Carlos Ghosn alifanyiwa uchunguzi Desemba 10, 2018 kwa kuficha mamlaka ya soko la hisa sehemu ya mapato yake yaliyopatikana kwa kampuni ya Nissan, sawa na yen bilioni 5 (sawa na euro milioni 38) kati ya mwaka 2010 na 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.