Pata taarifa kuu
JAPAN-GHOSN-UCHUMI-HAKI

Carlos Ghosn kuendelea kuzuiliwa hadi Januari 11

Mahakama ya Tokyo imeamua kuongeza muda wa kuzuiliwa kwa Carlos Ghosn, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Renault kwa siku nyingine 10, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Japan.

Bango lililowekwa picha kubwa ya Carlos Ghosn likiandikwa "Tunaungana na Carlos Ghosn" kwenye moja ya mitaa ya Beirut, Lebanon. Kampeni iliyozinduliwa nchini Lebanoni Desemba 6, 2018 ili kuonyesha uungaji mkono kwa gwiji huyo anayezuiliwa nchini Japan.
Bango lililowekwa picha kubwa ya Carlos Ghosn likiandikwa "Tunaungana na Carlos Ghosn" kwenye moja ya mitaa ya Beirut, Lebanon. Kampeni iliyozinduliwa nchini Lebanoni Desemba 6, 2018 ili kuonyesha uungaji mkono kwa gwiji huyo anayezuiliwa nchini Japan. JOSEPH EID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Carlos Ghosn anashtumiwa kosa la uvunjaji wa uaminifu. Kiongozi wa zamani wa kampuni ya magari Nissan anazuliwa tangu 19 Novemba.

Mapema mwezi Desemba Carlos Ghosn ameshtakiwa kwa kuficha mapato kwa kipindi cha miaka mitano. Carlos Ghosn yuko mikononi mwa vyombo vya sheria vya Japan tangu mwezi Novemba mwaka huu, akidaiwa kuhusika na tuhuma mbaya ya matumizi ya fedha za mwajiri wake.

Carlos Ghosn, mwenye umri wa miaka 64, mbali na kuwa mwenyekiti wa Nissan, pia ana wadhifa kama huo katika kampuni ya magari ya Mitsubishi na Mtendaji Mkuu wa kambuni ya magari ya Renault.

Miongoni mwa tuhuma zinazomkabli, ni kupotosha mshahara wake akidai anapokea pungufu na wakati huo huo akitumia mali ya kampuni kwa manufaa binafsi.

Kwa mujibu wa vyanzo vilio karibu ya kesi hiyo, Ghosn akiwa na mtendaji mwingine, Gerg Kelly, walikula njama kuanzia mwaka 2010 kufanya malipo ya fidia.

Kulingana na sheria za Japan, iwapo Ghosn atapatikana na hatia ya kughushi taarifa za kiusalama anaweza kuingia jela miaka 10, au kulipa faini ya Yen milioni 10.

Hivi karibuni mahakama ya Japan ilitangaza kwamba imekataa ombi jipya la kuongezwa muda wa kuzuiliwa Carlos Ghosn.

Kushikiliwa kwa gwiji huyo kwenye nafasi nyeti katika kampuni za magari, kumeleta mtikisiko katika sekta nzima ya uundaji wa magari

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.