Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Japan: Ofisi ya mashtaka ya Tokyo yamfungulia mashitaka Carlos Ghosn na kampuni ya Nissan

media Carlos Ghosn, Mwenyekiti wa kampuni za kutengeneza magari za Renault-Nissan, Oktoba 1, 2018. REUTERS/Regis Duvignau/File Photo

Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya kuunda magari ya Nissan nchini Japan Carlos Ghosn ameshtakiwa kwa kuficha mapato kwa kipindi cha miaka mitano. Carlos Ghosn yuko mikononi mwa vyombo vya sheria vya Japan tangu mwezi Novemba mwaka huu, akidaiwa kuhusika na tuhuma mbaya ya matumizi ya fedha za mwajiri wake.

Carlos Ghosn, mwenye umri wa miaka 64, mbali na kuwa mwenyekiti wa Nissan, pia ana wadhifa kama huo katika kampuni ya magari ya Mitsubishi na Mtendaji Mkuu wa kambuni ya magari ya Renault.

Miongoni mwa tuhuma zinazomkabli, ni kupotosha mshahara wake akidai anapokea pungufu na wakati huo huo akitumia mali ya kampuni kwa manufaa binafsi.

Kwa mujibu wa vyanzo vilio karibu ya kesi hiyo, Ghosn akiwa na mtendaji mwingine, Gerg Kelly, walikula njama kuanzia mwaka 2010 kufanya malipo ya fidia.

Kulingana na sheria za Japan, iwapo Ghosn atapatikana na hatia ya kughushi taarifa za kiusalama anaweza kuingia jela miaka 10, au kulipa faini ya Yen milioni 10.

Kushikiliwa kwa gwiji huyo kwenye nafasi nyeti katika kampuni za magari, kumeleta mtikisiko katika sekta nzima ya uundaji wa magari

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana