Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Zoezi la uokoaji kufuatia ajali ya ndege mbili za jeshi la Marekani laendelea

media ndege aina ya MV-22 ya Osprey. REUTERS/Kyodo

Zoezi kabambe la uokoaji linaendelea kwenye bahari ya Japan baada ya ndege mbili za jeshi la Marekani kugongana na kuanguka katika bahari hiyo. Vyanzo rasmi vinabaini kwamba ndege hizo zilikuwa na wanajeshi saba.

Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi, ndege hizo zilikuwa za KC-130 na F/A-18 kutoka kambi ya Iwakuni karibu na Hiroshima. Tayari wanajeshi kadhaa wameokolewa na kuna baadhi ambao wanaendelea vizuri, kwa mujibu wa chanzo hicho.

Kulikuwa na wanajeshi watano kwenye ndege ya C-130 na wawili kwenye ndege ya F-18. Mmoja wa wale waliookolewa alikuwa kwenye ndege ya kijeshi, kwa mujibu wa maafisa wa Japan.

Ndege ya KC-130 ni aina ya ile ya C-130 iliyoboreshwa na hutumiwa kungezea ndege zingine mafuta zikiwa hewani.

Vyombo vya habari vya Marekani vinasema ndege hizo zilianguka wakati wa kuongezwa mafuta zikiwa angani.

Jeshi la wanamaji halijathibitisha rasmi taarifa hiyo lakini limekitaja kisa hicho kuwa hitilafu.

Hata hivyo Marekani ina zaidi ya wanajeshi 50,000 walio nchini Japan, zaidi ya 18,000 kati yao wakiwa ni wanamaji.

Waziri wa ulinzi nchini Japan Takeshi Iwaya alisema ndege tisa za Japan na meli tatua zinashiriki katika oparesehni ya uokoaji.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana