Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-NATO-USALAMA

Mvutano kati ya Ukraine na Urusi: NATO kukutana na Kiev

"Kikao cha dharura" cha Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi (NATO) na Ukraine kinatarajia kufanyika leo Jumatatu alaasiri mjini Brussels kwa ombi la Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg.

Urusi inazuia tangu siku ya Jumapili, Novemba 25, meli tatu za kikosi cha wanamaji cha Ukraine.
Urusi inazuia tangu siku ya Jumapili, Novemba 25, meli tatu za kikosi cha wanamaji cha Ukraine. REUTERS/Pavel Rebrov
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unakuja baada ya Urusi kushikilia meli za Ukraine katika eneo la Kerch, eneo ambalo linaloingiliana na Bahari ya Azov.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amekubali kuitisha kikao cha dharura cha Jumuiya hiyo na Ukraine kwa ombi la rais wa Ukraine Petro Porochenko. Hata hivyo "mkutano huo utaajumuisha mabalozi Jumatatu hii alaasiri katika mji wa brussel, nchini Ubelgiji ili kujadili hali hiyo, " NATO imesema katika taarifa yake. Siku ya Jumapili tarehe 25 Novemba, Urusi ilizishikiliwa kwa nguvu meli tatu za jeshi la wanamaji la Ukriane, na hivyo kuwajeruhi baadhi ya askari katika eneo la Kerch, kitendo ambacho kimesababisha kuongezeka kwa mvutano mkubwa katika eneo hilo tete.

Sheria ya kivita

Usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii, Baraza la Usalama la Ukraine lilikutana kwa dharura na kupekeza kwa Rais Petro Poroshenko kuchukuwa sheria ya kivita "kwa siku 60."

Mvutano unaendelea katika eneo hilo tete, Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limeitisha kikao cha dharura leo Jumatatu alaasiri, kwa mujibu wa wanadiplomasia. Kikao ambacho kiliombwa na nchi hizo mbili. Katibu Mkuu wa NATO na Rais wa Ukraine walizungumzia leo Jumatatu kuhusu "hali hiyo, NATO imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.