Pata taarifa kuu
URUSI-JAPANI-USHIRIKIANO

Putin na Abe wazungumzia kuhusu mkataba wa amani

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe wamefanya mazungumzo leo Jumatano huko Singapore kuhusu mkataba wa amani kati ya nchi zao, ambazo bado ziko katika hali ya vita.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe huko Singapore tarehe 14 Novemba 2018.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe huko Singapore tarehe 14 Novemba 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tunatarajia kujadili si tu ushirikiano wa nchi zetu mbili, pia kiuchumi (...), lakini pia suala la mkataba wa amani," amesema Abe

"Niko tayari kutoa muda wa kutosha kwa suala hili, mkataba wa amani," amesema.

"Ninafurahi kuweza kuzungumza na wewe njia zote za ushirikiano wetu, ikiwa ni pamoja na yale ambayo wewe mwenyewe unaona kuwa ni vipaumbele," Putin amesema.

Mnamo mwezi Septemba, Vladimir Putin alitoa mapendekezo kwa Japani kufunika ukurasa wa Vita Kuu ya Pili kwa kutia saini "bila masharti" mkataba wa amani ifikapo mwishoni mwa mwaka.

Pendekezo, lililotolewa na Bw Putin kwa Bw Abe, katika kongamano la kiuchumi lililofanyika huko Vladivostok, hata hivyo, lilipokelewa shingo upande na Tokyo, ambayo inadai kurejeshewa visiwa vinne vilivyounganishwa na na Urusi ya zamani (USSR) mwaka 1945 .

Mkutano ujao kati ya viongozi hawa wawili umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba huko Argentina kando ya mkutano wa G20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.