Pata taarifa kuu
URUSI-NATO-USHIRIKIANO

Urusi yahadi kujibu dhidi ya mazoezi ya kijeshi ya NATO

Baada ya mazoezi makubwa ya kijeshi ya Urusi mnamo mwezi Septemba, wakati huu Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) inaendesha mazoezi makubwa ya kijeshi nchini Norway, hali ambayo imesababisha mvutano mkubwa.

Wakati wa mazoezi ya kijehi ya NATO yanayofahamika kwa jina la Trident Juncture 18, hapa ilikuwa Oktoba 19, 2018.
Wakati wa mazoezi ya kijehi ya NATO yanayofahamika kwa jina la Trident Juncture 18, hapa ilikuwa Oktoba 19, 2018. Kylee Ashton/U.S. Air Force/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tangu juma lililopita NATO inafanya mazoezi makubwa ya kijeshi nchini Norway, mazoezi ambayo Urusi imekosoa na kusema itajibu. Majeshi ya Urusi yametangaza nia yao ya kufanya mazoezi ya kurusha risasi na mabomu katika eneo la baharini karibu na eneowanakofanya mazoezi wezi majeshi ya NATO.

Tayari Urusi ilishtumu mazoezi ya hivi karibuni ya NATO kwa ushirikiano na Sweden na Finland nchini Norway kwamba ni ya uchukozi. Kwa mujibu wa Urusi,mazoezi hayo yanatishia utulivu wa kisiasa katika eneo la kaskazini na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema wako tayari kujibu dhidi ya mazoezi hayo ya NATO.

Jibu la Urusi linaendana na mazoezi ya kijeshi eneo la baharini la kimataifa kwenye Pwani ya Norway ambapo Urusi imetangaza mazoezi ya kurusha makombora.

Katibu Mkuu wa NATO na Waziri wa Ulinzi wa Norway, ambao wote wako katika eneo la mazoezi, wamejaribu kufutilia mbali madai hayo ya Urusi na kusema kwamba hali hii hutokea mara kwa mara na kwamba kauli hiyo ya Urusi haiwezi kubadili chochote mazoezi ya washirika.

Suala hili linatarajiwa kujadiliwa leo Jumatano katika makao makuu ya Muungano wa Atlantiki ambapo kutafanyika mkutano wa Baraza kati ya NATO na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.