Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANi-USHIRIKIANO

China yakanusha kuingilia siasa za ndani za Marekani

China imekanusha vikali madai ya Marekani kuwa inaingia siasa za nchi hiyo hasa wakati huu ikielekea katika Uchaguzi wa wawakilishi na Maseneta. Mvutano kati ya nchi hizi mbili unaendelea kuzua kizaaza.

Vita vya maneno vyaendelea kati ya Marekani na China.
Vita vya maneno vyaendelea kati ya Marekani na China. REUTERS/Damir Sagolj/
Matangazo ya kibiashara

Madai hayo yametolewa na Makamu wa rais Mike Pence, ambaye amesema China inaunga mkono wanasiasa wanaompinga rais Donald Trump kutokana na msimamo wake mkali kuhusu maswala ya biashara, huku akisisitiza kuwa China inamtaka rais mwingine wa Marekani.

“Beijing inafanya kampeni ya kumdharau rais Trump na kuiangusha ajenda yetu, na mambo tunayoamini, wakati huu tunapozungumza, Beijing inatumia mbinu mbalimbali ili kuingilia maswala yetu ya ndani na siasa za Marekani, ” amesema Mike Pence.

“ Kuweka wazi, uongozi wa rais Trump unafanya kazi, na China inamtaka rais mwingine wa Marekani, hakuna shaka kuwa China inaingilia mambo ya ndani ya Marekani,” ameingeza Makamo wa rais wa Marekani.

Hata hivyo China imefutilia mbali madai hayo ikisema kuwa ni shutma zisizokuwa na msingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.