Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-ULINZI-USHIRIKIANO

Marekani yaiwekea vikwazo China kwa kununua silaha za Urusi

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya China, baada ya kununua silaha za kijeshi kutoka Urusi. Hata hivyo Urusi umefutilia mabli madai hayo ya Marekani.

Polisi wa China wakifanya mazoezi katika eneo la Tiananmen Machi 3, 2017. Maelfu ya polisi, askari na watu wanaojitolea wakizingira mji wa Beijing.
Polisi wa China wakifanya mazoezi katika eneo la Tiananmen Machi 3, 2017. Maelfu ya polisi, askari na watu wanaojitolea wakizingira mji wa Beijing. REUTERS/Tyrone Siu
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Marekani inasema hatua hii inakiuka vikwazo vilivyowekewa Urusi mwaka 2014 kuuza silaha zake kutoka na uvamizi wa Ukraine lakini pia kwa madai ya kuingilia siasa za Marekani.

Hata hivyo, China imesema haijawahi kuunga mkono vikwazo hivyo vilivyowekwa na Marekani na washirika wake kutoka barani Ulaya.

Beijing ilinunua ndege 10 za kivita pamoja na makombora ya masafara marefu aina ya S-400.

Uhusiano kati ya Marekani na Urusi umeendelea kuwa mbaya tangu mwaka 2014 ilipoamua kuchukua eneo la Crimea huko Ukraine na madai ya kuingilia Uchaguzi Mkuu mwaka 2016.

Madai hayo yote hayo yamekuwa yakikanushwa na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.