Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
Asia

Korea Kaskazini na Kusini zakubaliana kuanza ushirikiano mpya

media Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akiwa katika mkutano na mwenyeji wake, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un jijini Pyongyang, Septemba 18, 2018. Pyeongyang Press Corps/Pool via REUTERS

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wamesaini makubaliano mbalimbali ya kusaidia kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

Miongoni mwa makubaliano hayo ni pamoja na namna ya Korea Kaskazini kuachana kabisa na mradi wake wa nyuklia, ambao umeendelea kutishia usalama wa Korea Kusini.

Korea Kaskazini pia imekubali kuachaana na majaribio ya makombora yake, ambayo yamekuwa yakionekana kutishia usalama wa Korea Kusini.

Kiongozi wa Korea Kaskazini amesema anatarajia kuzuru Korea Kusini hivi karibuni.

Mkutano huu umefuata ule uliofanyika mwezi Juni, baada ya viongozi hao wawili kukutana mpakani, lakini pia Kim Jong Un kukutana na rais wa Marekani nchini Singapore.

Kukutana kwa viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini, kumeleta matumaini ya kuimarika tena kwa uhusiano kati ya nchi hizo jirani.

 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana