Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Tetemeko la ardhi laua watu 44 Japani

media Timu ya waokoaji kutoka kikosi cha polisi ya Japani huko Astuma, mji ulioathiriwa na tetemeko la ardhi kaskazini mwa Japan, Septemba 9, 2018. © AFP

Tetemeko kubwa la ardhi lililopiga wiki jana kisiwa cha Hokkaido, kaskazini mwa Japani limeua watu 44 na hakuna mtu ambaye alitoweka, serikali imetangaza Jumatatu wikii.

Takribani waokoaji 40,000 (maafisa wa Zima Moto, polisi, askari) wamekua wakiendelea na kutoa msaada kwa wakazi wa kisiwa hicho, ambapo zaidi ya watu 2,700 wameyahama makaazi yao.

Vifo vingi vimeoripotiwa katika kijiji cha Atsuma, ambako nyumba zilifunikwa kwa matope kutokana na tetemeko lenye ukubwa wa 6.6 katika vipimo vya Richter.

"Serikali itachukua hatua zote zinazohitajika ili kila mtu aweze kurudi katika maisha ya kawaida na salama haraka iwezekanavyo," msemaji wa serikali, Yoshihide Suga amesema katika mkutano na waandishi wa habari wa kila siku.

Pia ametoa wito kwa raia kuwa makini, wakati mvua zinatarajiwa kunyesha katika eneo hilo, hali ambayo inaweza kusababisha kutiririka kwa matope.

Waziri Mkuu Shinzo Abe, ambaye alizuru siku ya Jumapili eneo hilo lililokumbwa na tetemeko la ardhi, aliahidi "kufanya kilio chini ya uwezo wake" ili kurekebisha maeneo yaliyoathirika na majanga ya asili ya hivi karibuni.

Kabla ya tetemeko hilo la ardhi la Hokkaido, eneo la magharibi ya nchi lilipigwa na dhoruba kali ambayo iliua watu 11 na kusababisha kufungwa kwa uwanja wa ndege wa Kansai (Osaka).

Mapema Julai, kisiwa hiki pia kilikumbwa na mvua kubwa ambazo zilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi, na kuua watu zaidi ya 220.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana