Pata taarifa kuu
KAMBODIA-SIASA-HAKI

Kiongozi wa upinzani aachiliwa huru Cambodia

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Cambodia, Kem Sokha, 65, ameachiliwa huru kwa dhamana baada ya kuzuiliwa jela kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa kushtumiwa kosa la uhaini, msemaji wa serikali ametangaza Jumatatu wiki hii.

Kem Sokha, mnamo mwaka 2017 katika jimbo la Prey Veng (Picha ya kumbukumbu).
Kem Sokha, mnamo mwaka 2017 katika jimbo la Prey Veng (Picha ya kumbukumbu). REUTERS/Samrang Pring/File Picture
Matangazo ya kibiashara

Mamia kadhaa ya wafuasi wake wamekusanyika nje ya nyumba yake.

"Ameachiliwa kwa dhamana na yuko chini ya udhibiti wa mahakama," msemaji wa serikali, Phay Siphan, amesema.

Kwa mujibu wa Kem Monovithya, binti wa Kem Sokha, baba yake aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani. Amesema baake yuko katika afya mbaya baada ya kiwango cha sukari kupanda katika na pia anahitaji upasuaji kwenye bega la kushoto.

Kem Sokha, mkuu wa chama cha Cambodia National Rescue Party (PSNC), ambaye amekataa tamaa, alikuwa kizuizini tangu mwzi Septemba mwaka 2017 kwa kushtumiwa kosa uhaini. Tangu wakati huo alikua kizuizini na kwekwa kando pekee karibu na mpaka wa Cambodia na Vietnam.

Waziri Mkuu Hun Sen alikuwa amekabiliwa na shinikizo la kumuachilia huru Kem Sokha baada ya uchaguzi wa bunge mwezi Julai, ambao chama chake cha CPP kilishinda, chama ambacho hakina mpianzani katika Bunge.

Chama cha PSNC kilifutwa mwaka jana na Mahakama Kuu na wanachama wake 118 wamenyimwa haki zao za kiraia kwa kipindi cha miaka mitano.

Kiongozi wa zamani wa chama cha PSNC Eng Chhai Eang na Makamu wa zamani wa rais Mu Sochua, wamethibitisha kwamba Kem Sokha sasa yuko nyumbani kwake.

Mamia ya wafuasi na waandishi wa habari walikusanyika nje ya nyumba yake huko Phnom Penh. Milango bado imefungwa. Mmoja wa wanasheria wake amesema kuwa "kwa mazingira hayo" kiongozi huyo wa upinzani hawezi kukutana na wafuasi wake kwa sasa.

Wapinzani kumi na wanne wa serikali waliachiliwa huru mwezi uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.