Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Seoul na Pyongyang kuzungumza kabla ya mkutano wa marais

media Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakisabahiana baada ya kumalizi kwa mkutano wao wa kihistoria katika jiji la Panmunjom, Korea ya Kaskazini, Mei 26, 2018. The Presidential Blue House /Handout via REUTERS

Wawakilishi kutoka Seoul na Pyongyang wanakutana Jumatatu wiki hii kwa mazungumzo ya ngazi ya juu, kabla ya mkutano kati ya viongozi wa pande zote mbili za rasi ya Korea, gazeti la kila siku la Korea Kusini la Kookmin Ilbo limeripoti.

Kim Jong-un, kiongozi wa Korea Kaskazini, na Moon Jae-in, rais wa Korea Kusini, walikutana mwezi Aprili na walikubaliana kuandaa mkutano katika majira ya baridi huko Pyongyang.

Gazeti la kila siku la Kookmin Ilbo likinukuu afisa mwandamizi wa Korea Kusini, limeripoti kwamba mkutano huo unatarajiwa kufanyika kabla ya mwishoni mwa mwezi Agosti.

Msemaji wa Moon Jae-in alisema siku ya Jumapili kuwa ofisi ya rais wa Korea Kusini ina imani kuwa tarehe ya mkutano huo inaweza kujadiliwa Jumatatu wiki hii.

"Tunatarajia kuwa tarehe, eneo na wajumbe katika mkutano huo wa kihistoria vinaweza kujadiliwa leo Jumatatu," msemaji wa rais amesema bila kutoa maelezo zaidi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana