Pata taarifa kuu
INDONESIA-MAJANGA YA ASILI

Tetemeko la ardhi laua watu 319 Indonesia

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi huko Lombok, nchini Indonesia imeendelea kuongezeka na sasa imefikia watu 319.

Msikiti wa Jamiul Jamaa, ulianguka kutokana na tetemeko la ardhi, ambako askari na maafisa wa Zima Moto wanatafuta watu waliofukiwa na udongo huko Pemenang, kaskazini mwa Lombok, Agosti 8, 2018.
Msikiti wa Jamiul Jamaa, ulianguka kutokana na tetemeko la ardhi, ambako askari na maafisa wa Zima Moto wanatafuta watu waliofukiwa na udongo huko Pemenang, kaskazini mwa Lombok, Agosti 8, 2018. Antara Foto/Zabur Karuru/ via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Ripoti ya hivi karibuni inasema kuwa watu 319 wamepoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi, " amesema katika mkutano na waandishi wa habari Waziri wa Usalama, Wiranto Awali ilitangazwa kwamba watu idadi ya watu waliopoteza maisha imefikia 164.

Maelfu ya watu wamejeruhiwa vibaya na watu 270,000 wameyahama makaazi yao, msemaji wa taasisi inayokabiliana na majanga, Sutopo Purwo Nugroho, amesema jioni.

Tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.9 kwenye vipimo vya Richter siku ya Jumapili, hili la Alhamisi limesababisha vifo vingi, ameongeza Sutopo Purwo Nugroho.

Tetemeko hili limesikika pia katika kisiwa jirani cha Bali, kinachotembelewa na watalii wengi Kusini-Mashariki mwa Asia.

Katika Kisiwa cha Lombok, "majengo kadhaa yameharibiwa na watu 24 walijeruhiwa kutokana na maporomoko ya taka taka," Sutopo amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.