Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Tetemeko la ardhi laua watu 319 Indonesia

media Msikiti wa Jamiul Jamaa, ulianguka kutokana na tetemeko la ardhi, ambako askari na maafisa wa Zima Moto wanatafuta watu waliofukiwa na udongo huko Pemenang, kaskazini mwa Lombok, Agosti 8, 2018. Antara Foto/Zabur Karuru/ via REUTERS

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi huko Lombok, nchini Indonesia imeendelea kuongezeka na sasa imefikia watu 319.

"Ripoti ya hivi karibuni inasema kuwa watu 319 wamepoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi, " amesema katika mkutano na waandishi wa habari Waziri wa Usalama, Wiranto Awali ilitangazwa kwamba watu idadi ya watu waliopoteza maisha imefikia 164.

Maelfu ya watu wamejeruhiwa vibaya na watu 270,000 wameyahama makaazi yao, msemaji wa taasisi inayokabiliana na majanga, Sutopo Purwo Nugroho, amesema jioni.

Tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.9 kwenye vipimo vya Richter siku ya Jumapili, hili la Alhamisi limesababisha vifo vingi, ameongeza Sutopo Purwo Nugroho.

Tetemeko hili limesikika pia katika kisiwa jirani cha Bali, kinachotembelewa na watalii wengi Kusini-Mashariki mwa Asia.

Katika Kisiwa cha Lombok, "majengo kadhaa yameharibiwa na watu 24 walijeruhiwa kutokana na maporomoko ya taka taka," Sutopo amesema.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana