Pata taarifa kuu
INDONESIA-MAJANGA YA ASILI

Mamia ya watu wakwama kwenye Mlima Rinjani Lombok

Maafisa wa uokoaji wako njiani kutoa msaada kwa mamia ya watu waliokwama kwenye mlima Rinjani tangu tetemeko kubwa kupiga kisiwa cha Lombok siku ya Jumapili, taasisi ya kukabiliana na majanga ya Indonesia imesema.

Wapanda mlima wa Idonesia na wale kutoka nchi za kigeni baada ya kupewa msaada wa kushuka kutoka Mlima Rinjani hadi Kijiji cha Sembalun huko Lombok Timur.
Wapanda mlima wa Idonesia na wale kutoka nchi za kigeni baada ya kupewa msaada wa kushuka kutoka Mlima Rinjani hadi Kijiji cha Sembalun huko Lombok Timur. REUTERS/Ahmad Subaidi
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.4 katika vipimo vya Richter limesababisha vifo vya watu wasiopingua 16, ambapo vifo vya watu wawili kati yao vimepotiwa leo Jumatatu. Tetemeko hilo pia limesababisha uharibifu mkubwa kwenye kisiwa hiki cha utalii, mashariki mwa Bali.

Chanzo cha tetemeko hilo kilikuwa karibu na Mlima wa Rinjani, volkano ya pili kwa ukubwa nchini Indonesia (mita 3,726) na moja ya vivutio vikuu vya Lombok.

Hifadhi ya mlima Rinjani,imefungwa kutokana na maporomoko ya ardhi.

Kisiwa hicho huwavutia watalii kutoka duniani kote kutokana na fukwe zake za kuvutia na maeneo ya kutembea, eneo hilo liko umbali wa kilometa 40 mashariki mwa Bali.

Zaidi ya watu 160 wamejeruhiwa na maelfu ya makazi yameharibiwa, maafisa wameeleza.

Sutopo Purwo Nugroho, Msemaji wa taasisi ya kukabiliana na majanga, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba watu 620 kwa jumla ya 820 waliokuepo kwenye mlima huo wakati wa tetemeko hilo walikuwa wageni na kwamba 246 kati yao waliondolewa Jumapili.

Helikopta mbili zilishiriki zoezi hilo wapiganaji zimekua zikipeleka chakula kwa wale waliokwama.

"Habari za hivi karibuni kutoka kwa timu zetu kwenye eneo la tukio zinaonyesha kuwa familia zilizokwama kwenye Mlima Rinjani zitaondolewa leo," amesema afisa mwandamiozi wa taasisi ya kukabiliana na majanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.