Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Njia bora ya kuwaokoa wavulana 12 na kocha wao yatathminiwa thailand

media Wavulana 12 walio na umri ulio chini ya miaka 16 na kocha wao wanasubiri kuokolewa baada ya kukwama katika pango.inside a flooded cave in Chiang Rai, Thailand, July 3, 2018, in this still image taken from a Thai Navy Seal handout video. ©hai Navy Seal Facebook/Handout via Reuters

Waokoaji nchini Thailand kwa sasa wanatathmini njia iliyo bora zaidi watakayotumia kufanikisha kuwaokoa wavulana 12 na kocha wao waliokwamba katika pango hadi seheme ya usalama.

Waokoaji nchini Thailand wanasema, hawatalazimika kuhatarisha maisha ya wavulana hao kocha wao, waliokwama ndani ya handaki kwa zaidi ya siku 10 sasa.

Wavulana hao wamepokea chakula kwa mara ya kwanza pamoja na dawa, baada ya waokoaji kufika katika handaki hilo.

Watalaam kutoka mataifa mbalimbali kwa sasa wanaendelea kuthathmini namna ya kuwaokoa, huku maombi yakiwa kuwa mvua kubwa haitaendelea kunyesha na kutatiza juhudi za kuwaokoa.

Wachezaji hao walikwenda kwenye handaki hilo kufanya mazoezi lakini, viwango vya maji viliongezeka na hivyo wakashindwa kuondoka.

Mvua nyingi zinazonyesha zinaashiria kiwango cha maji kujaa na kuhatarisha maisha ya watu waliomo pangoni pamoja na mifuko ya hewa waliyonayo mahali waliko kama mateka.

Wavulana hao waligunduliwa siku tisa baada ya kuingia pangoni humo huko katika jimbo la Chiang Rai kufuatia mafunzo ya mpira waliyokuwa wakifanya na kujikuta wakikwama pangoni kutokana na kina cha maji kuongozeka kulikosababisha na mvua nyingi zinazonyesha.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana