Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 07/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Kim Jong afanya ziara ya kushtukiza China

media Picha ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un iliyotolewa na shirika la habari la Korea Kaskazini Kcna Juni 13, 2018 alipofika uwanja wa ndege wa Pyongyang baada ya mkutano na Rais wa Marekani Donald Trump huko Singapore. AFP

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong amefanya ziara ya kushtukiza nchini China na kupokelewa na mwenyeji wake Xi Jinping, wiki moja baada ya mkutano wa kihistoria kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini na Rais wa Marekani Donald Trump.

Televisheni ya China imerusha picha za mkutano kati ya viongozi hao wawili na wake zao katika sherehe ya mapokezi iliyofanyika katika ikulu ya rais.

Ziara hii ya kushtukizaimefanyika wakati ambapo China imekua katika mvutano mkubwa na rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani, mvutano ambao umesababisha Jumanne wiki hii kushuka kwa masoko ya hisa duniani.

Hii ni ziara ya tatu ya kiongozi wa Korea Kaskazini nchini China katika kipindi kisichozidi miezi mitatu. Mwishoni mwa mwezi Machi, Bw Kim alifanya ziara yake ya kwanza nje Korea Kaskazini tangu alipochukua hatamu ya uongozi mwishoni mwa mwaka 2011, kabla ya safari ya pili mnamo mwezi Mei katikamji wa Dalian kaskazini mashariki mwa China.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana