Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KUSINI-JAPAN-USALAMA

Japan: Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini yalikua muhimu

Saa chache baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kusitisha mpango wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi na nchi ya Korea Kusini, Serikali ya Japan imeeleza wasiwasi wake kutokana na uamuzi huo, ikisisitiza kuwa mazoezi hayo yalikuwa muhimu kwa usalama.

Korea Kusini na Marekani mara kwa mara hufanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja. Hapa ilikua Aprili 26, 2017 huko Pocheon.
Korea Kusini na Marekani mara kwa mara hufanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja. Hapa ilikua Aprili 26, 2017 huko Pocheon. JUNG Yeon-Je / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne baada ya mkutano wake wa kihistoria na Kim Jong Un, rais Trump alisema hakuna haja ya mazoezi hayo aliyosema yanaigharimu fedha nyingi nchi yake na kukiri kuwa ni uchokozi kwa Korea Kaskazini.

Licha ya wadadisi wengi kuona kuwa Marekani haijafanikiwa katika mkutano huu, rais Trumo mwenyewe akiongea na wanahabari kabla ya kurejea Washington amesema Korea Kaskazini imekubali kuachana na mpango wake wa nyuklia.

Magazeti mengi ya Korea Kaskazini kikiwemo kituo cha taifa cha televisheni vimeripoti kuwa rais Trump amekubali kuiondolea vikwazo nchi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.