Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Mkutano wa Singapore: Donald Trump na Kim Jong-un wasaini hati ya pamoja

media Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakisaini hati ya pamoja katika Hoteli ya Capella katika kisiwa cha Sentosa Island, Singapore, Juni 12, 2018. REUTERS / Jonathan Ernst

Baada ya vita vya maneno na vitisho vingi vya kufuta mkutano kutoka kila upande, hatimaye mkutano wa kihistoria kati ya Marekani na Korea Kaskazini umefanyika huko Sentosa nchini Singapore Jumanne hii, Juni 12.

Mkutano huo umeanza saa tatu saa za Singapore baada ya kubadilishana maneno ya busara na kushikana mikono katika tukio la kihistoria wakati huu viongozi hawa wakimaliza awamu ya kwanza ya mazungumzo ya awali nchini Singapore. Mkutano huu wa ana kwa ana ni wa kwanza katika historia kati ya viongozi hawa nchi ambazo kwa miongo kadhaa katika uhasama.

Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili hao pekee na wakalimani wao.

Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama katika rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.

Kwa upande wa Donald Trump, anasema hatua ya kutokomeza silaha za nyuklia itaanza "haraka sana". Rais wa Marekani anasema ameanzisha "uhusiano maalum" na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

Wakati huo huo China imepongeza mwanzo wa 'historia mpya' kati ya Marekani na Korea Kaskazini baada ya tukio hilo la kihistoria.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana