Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-USHIRIKIANO

Ukraine yastumiwa kutoa madai ya uongo kuhusu mauaji ya mwanahabari

Mwandishi wa habari wa Urusi Arkady Babchenko, ambaye vyombo vya usalama vya Ukraine vilidai aliuawa Jumanne wiki hii, bado yuko hai.

Mwandishi wa Urusi Arkadi Babchenko (katikati) akikutana na Rais wa Ukrainei Petro Poroshenko (kushoto) Mei 30, 2018.
Mwandishi wa Urusi Arkadi Babchenko (katikati) akikutana na Rais wa Ukrainei Petro Poroshenko (kushoto) Mei 30, 2018. Mykola Lazarenko/Ukrainian Presidential Press Service/Handout vi
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa polisi kutoka Ukraine ambaye hakutaka kutaja jina lake, kwa kuhofia usalam wake amesema Arkady Babchenko alipotezwa na vikosi vya usalama Ukrain (SBU) kwa minajili ya kuendesha "operesheni maalum" na kuwakamata watu watakaosingiziwa mauaji hayo ya uongo.

Hata hivyo serikali ya Ukraine, imeshtumiwa kwa kutoa ripoti za uongozi kuhusu kuuawa kwa mwanahabari wa Urusi Arkady Babchenko, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin.

Shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya, limesema Ukraine imesambaza habari za uongo huku Shirika linalotetea wanahabari duniani, likisema, kilichotokea ni vita vya habari.

Ukraine imejitetea kwa kusema kuwa ilikuwa inazuia uwezekano wa mwanahabri huyo kuuawa, huku Urusi ikisema imechokozwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.