Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini yamtusi makamu wa rais wa Marekani

Nchi ya Korea Kaskazini imemjia juu makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, ikimuita kiongozi huyo “mjinga na asiye na maarifa” wakati huu utawala wa Pyongyang ukitishia kujitoa kwenye mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.

Korea Kaskazini imemuita Mike Pence mjinga kwa kuifananisha Korea Kaskazini, taifa la nyuklia na Libya, ambayo alisema ilikuwa na vifaa vichache tu ilivyokuwa ikicheza navyo.
Korea Kaskazini imemuita Mike Pence mjinga kwa kuifananisha Korea Kaskazini, taifa la nyuklia na Libya, ambayo alisema ilikuwa na vifaa vichache tu ilivyokuwa ikicheza navyo. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui, amesema matamshi ya Pence ya hivi karibuni hayakupaswa kutolewa na kwamba kama haitaki mazungumzo nchi yao iko tayari kurejelea mpango wake wa nyuklia.

Korea Kaskazini imesema itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia.

Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ametupilia mbali uwezekano wa kutofanyika kwa mazungumzo hayo, akisema mwenye usemi wa mwisho ni Kim Jong-un.

Matamshi haya ya Korea Kaskazini yanakuja siku chache tu tangu rais Trump asema kuwa kuna uwezekano mkutano wake na Kim Jong-un usifanyika katika tarehe iliyopangwa nchini Singapore.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.