Serikali ya Korea Kaskazini imealika waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali thelathini tano: Marekani, China, Urusi, Korea Kusini na Uingereza.
Wamekuja kuhudhuria milipuko hiyo ya kuharibu vituo hivyo vya majaribio, Kaskazini-Mashariki mwa nchi, kwenye kituo hicho kikuu, kwenye mlima, ambapo serikali ilitekeleza milipuko sita ya kinyuklia tangu mwaka 2006 hadi mwaka jana.
Lakini waandishi hawa wa habari wa kigeni wako chini ya uangalizi mkali na hawana uwezo wowote wa kuendesha kazi halisi ya uchunguzi.
Baada ya kuwasili kwao katika Uwanja wa Ndege wa Wonsan, simu zao na vifaa vyao mbalimbali vimechukuliwa na mamlaka husika, amesema mwandishi kutoka kituo cha Sky News kutoka Uingereza.