Pata taarifa kuu
ARMENIA-SIASA

Bunge kumchagua Waziri Mkuu mpya Armenia

Bunge la Armeia linakutana Jumanne wiki hii kuchagua Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, inayokabiliwa kwa wiki tatu mfululizo na maandamano dhidi ya serikali. Kiongozi wa maandamano hayo Nikol Pashinian ni mgombea pekee anayewania nafasi hiyo.

Kiongozi wa upinzani Nikol Pachini akizungumza mbele ya wabunge wakati wa kikao cha bunge cha Mei 1 huko Yerevan.
Kiongozi wa upinzani Nikol Pachini akizungumza mbele ya wabunge wakati wa kikao cha bunge cha Mei 1 huko Yerevan. REUTERS/Vahram Baghdasaryan/Photolure
Matangazo ya kibiashara

Mbunge wa upinzani na mwandishi wa habari wa zamani Nikol Pachini, mwenye umri wa miaka 42, anawania nafasi ya waziri mkuu kwa mara ya pili ndani ya siku nane, baada ya kushindwa wiki iliyopita.

Tarehe 1 Mei, wakati pia alikuwa mgombea pekee, alishindwa kukusanya kura 53 zilizohitajika kwa jina lake, wapinzani wake kutoka Chama cha Republican madarakani, ambacho kina viti 58 kati ya 105, walipiga kura dhidi yake.

Lakini siku moja baada ya kushindwa kwake, alihakikisha kuwa ana kura za kutosha kuchaguliwa, akisema kuwa "makundi yote (wabunge) walisema kuwa watamuunga mkono" kwenye nafasi ya waziri mkuu.

Waziri mkuu katika nchi hiyo ya Urusi ya zamani ana mamlaka makubwa baada ya marekebisho ya katiba, wakati ambapo rais anafanya kazi za heshima.

Kwa mujibu wa wachambuzi waliohojiwa na shirika la habari la AFP, wabunge wa chama tawala walichukua hatua hiyo ili kuendelea kuimarisha udhibiti wao wa Bunge, lakini kuna hatari ya bunge hilo kuvunjwa kama litashindwa kuchagua Waziri Mkuu kwa mara ya pili mfululizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.