Pata taarifa kuu
INDIA-HAKI

Muigizaji nguli Salman Khan kufungwa jela miaka mitano

Nchini India, kesi ya muigizaji maarufu Salman Khan imeendelea kugonga vichwa vya habari nchini India, baada ya mahakama kumuhukumu kifungo cha miaka mitano. Mahakama nchini India imemhukumu Salman Khan, kifungo cha miaka mitano jela baada ya kumkuta na hatia ya kufanya ujangili na kumuua swala paa kinyume cha sheria mnamo mwaka 1998.

Muigizaji maarufu wa sauti Salman Khan (amevalia shati nyeusi)) akiwasilia mahakamani jodhpur, Rajasthan, magharibi mwa India, tarehe 5 Aprili, 2018.
Muigizaji maarufu wa sauti Salman Khan (amevalia shati nyeusi)) akiwasilia mahakamani jodhpur, Rajasthan, magharibi mwa India, tarehe 5 Aprili, 2018. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Salman Khan ni mmoja wa waigizaji ghali kumi duniani, na hii si mara ya kwanza kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, ikiwa ni pamoja na tuhuma za unyanyasaji nyumbani au kwa kifo cha mtu asiye na makazi.

Mbali na hukumu hiyo ya kifungo jela, mahakama pia imempiga faini ya Repee 10,000 (sawa na dola 154). Khan amechukuliwa kupelekwa gerezani muda mfupi uliopita.

Waigizaji wengine wanne waliokuwa naye wakati wa tukio hilo ambao waliunganishwa kwenye kesi hiyo wameachiwa huru.

Khan mwenye umri wa miaka 52 ambaye filamu zake zimevuka mipaka ya Hollywood na kuteka kona nyingi za dunia, anayo nafasi ya kukata rufaa kwenye mahakama kuu.

Hii ni kesi ya nne aliyowahi kufunguliwa muigizaji huyo kwa madai ya kufanya ujangili dhidi ya wanyama pori alipokuwa anatayarisha filamu yake ya Hum Saath Saath Hain, mwaka 1998.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.