Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Serikali mpya ya Bolivia yamtambua Guaido kama rais wa Venezuela (waziri)
Asia

China na Korea Kaskazini zaonesha umoja baada ya ziara ya Kim

media Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa na mwenyeji wake rais wa China Xi Jingping. CCTV via Reuters

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong amefanyiwa hafla ya kipekee na mwenyeji wake rais wa China Xi Jinping wakati alipofanya ziara ya siri jijini Beijing wakati huu nchi hizo mbili zikikubaliana kuboresha uhusiano wao.

Ziara ya Kim Jong-Un imefanyika wakati huu ambapo anatarajiwa pia kuwa na mkutano na viongozi wa Korea Kusini pamoja na rais wa Marakani Donald Trump.

Katika ziara yake ya kwanza tangu aingie madarakani, Kim akiambatana na mke wake walipokelewa kwa gwaride la heshima na kufanyiwa sherehe na rais Xi, kimeripoti kituo cha taifa cha habari ambacho kimeongeza kuwa haikuwa ziara rasmi ambapo ilithibitishwa baada ya Kim kurejea nchini mwake Jumatano ya wiki hii.

Viongozi hao wawili walifanya mazungumzo kwenye ofisi ya Great Hall ya chama tawala ambapo kwa pamoja wamepongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya mataifa huku Kim akiahidi nchi yake kuachana na mpango wake wa nyuklia.

“Hakuna swali kuwa ziara yangu ya kwanza ya nje ya nchi itakuwa ni China,” alisema Kim wakati alipohojiwa na kituo cha televisheni cha nchi yake KCNA.

“Huu ni wajibu wangu kama mtu mwingine yeyote ambaye anapaswa kuheshimu matunda ya uhusiano wa nchi yetu na China kwa vizazi na vizazi.”

KCNA imesema kuwa rais wa china Xi Jinping amekubali mualiko wa mgeni wake kutembelea Pyongyang, ziara ambayo itakuwa ni ya kwanza nchini Korea Kaskazini tangu nayeye aingie madarakani mwaka 2012.

Viongozi hawa walikuwa hawajawahi kukutana tangu Kim aingie madarakabi baada ya kifo cha baba yake Kim Jong Il mwaka 2011, lakini uhusiano wa nchi hizo mbili uliingia dosari tangu China iwe inaunga mkono maazimio ya umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo.

Hata hivyo rais wa China Xi ameeleza umuhimu wa nchi hizo mbili kushirikiana akisema “Kim amefanya uchaguzi sahihi na chaguo makini” na kwamba yuko tayari kuendelea kuwasiliana mara kwa mara na Kim “katika muktadha mpya.”

Rais Xi na Kim walionekana kushikana mkono na kukaa bega kwa bega katika muda wote wa mikutano yao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana