Pata taarifa kuu
URUSI

Urusi: Watu 53 wakiwemo watoto wapoteza maisha kwenye ajali ya moto

Watu 53 wamethibitishwa kufa wakati moto ulipounguza duka moja la jumla katikati ya mji wa viwanda Siberia nchini Urusi, wakati huu watu wengi wakiwa hawajulikani walipo wakiwemo watoto, idara ya usalama imesema.

Vikosi vya uokoaji vikiendelea na juhudi za kuzima moto kwenye duka moja kubwa Siberia, Urusi ambako watu 53 wamepoteza maisha. 26 Machi 2018.
Vikosi vya uokoaji vikiendelea na juhudi za kuzima moto kwenye duka moja kubwa Siberia, Urusi ambako watu 53 wamepoteza maisha. 26 Machi 2018. REUTERS/Dmitry Saturin
Matangazo ya kibiashara

Picha za kituo cha televisheni ya Urusi zimeonesha moshi mweusi ukiendelea kufuka kutoka kwenye duka hilo lililoko kwenye mji wa Kemerovo, duka ambalo pia linatoa huduma za Sauna, Bowling na majumba kadhaa ya Sinema.

“Watu 53 wamethibitishwa kufa,” amesema msemaji wa timu ya kamati ya wachunguzi ya Urusi, Svetlana Petrenko.

Idadi ya awali ya watu walipoteza maisha ilikuwa watu 39 huku 69 wakiwa hawajulikani wakiwemo watoto 40.

Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa moto huo ulianza majira ya satano asubuhi kwenye ukumbi mmoja wa Sinema.

Kamati ya uchunguzi imesema kuwa paa la kumbi za sinema lilianguka na kufunika watu wengi waliokuwemo.

Polisi wanasema moto ulianzia kwenye ghorofa ya tatu ya jengo hilo na vikosi vya uokoaji vimeendelea kuudhibiti na kuondoa matofali na machuma yaliyoanguka.

Kamati ya uchunguzi ya Urusi imesema itafungua jalada la uchunguzi na watu wanne akiwemo mpangaji ambaye moto ulianzia kwenye ofisi yake na mkuu wa kampuni inayomiliki maduka hayo tayari amekamatwa.

Watu zaidi ya 120 walifanikiwa kuokolewa kutoka kwenye jengi hilo, wamesema maofisa wanaoshiriki zoezi la uokoaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.