Pata taarifa kuu
CHINA-SIASA-UONGOZI

Bunge labadilisha Katiba kumfanya Xi Jingping kuwa rais wa maisha.

Juhudi za wapigania Demokrasia nchini China huenda sasa zikawa zimekufa rasmi baada ya mwishoni mwa juma bunge la nchi hiyo kuidhinisha mabadiliko ya katiba yanayomfanya rais Xi Jingping kuwa rais wa maisha.

Rais wa China  Xi Jinping wakati wa kupiga kura kuibadilisha Ktiba Machi 11 2018
Rais wa China Xi Jinping wakati wa kupiga kura kuibadilisha Ktiba Machi 11 2018 ©REUTERS/Jason Lee
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa bunge umemaliza rasmi utaratibu wa kubadilishana madaraka uliokuwa umepigiwa chapuo na kiongozi wa zamani marehemu Deng Xiaoping baada ya kushuhudia kwa muda mrefu nchi hiyo ikiongozwa na mtu mmoja ambaye alikuwa muasisi wa chama cha kikomunist Mao Zedong.

Wakati wa zoezi la kupiga kura kuidhinisha mabadiliko hayo vyombo vya habari havikuruhusiwa katika uamuzi ambao sasa unazima rasmi harakati za vuguvugu la eneo la Hong Kong.

Uamuzi huu unaelezwa na wachambuzi wa siasa za Kimataifa kuwa, China inajaribu kuonesha dunia kuwa, demokrasia kwao sio kubadilishana vongozi kama ilivyo katika mataifa ya Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.