Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI

Trump akubali kufanya mazungumzo na Kim Jong Un

Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kukutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kabla ya mwezi Mei mwaka huu kujadiliana kuhusu mradi wake wa nyuklia ambao Jumuiya ya Kimataifa unasema  unahatarisha amani ya dunia.

Chung Eui-yong, mshauri wa maswala ya usalama wa Korea Kusini baada ya kukutana na rais wa Marekani Donald Trump Mei 8 2018 katika Ikulu ya Whote House
Chung Eui-yong, mshauri wa maswala ya usalama wa Korea Kusini baada ya kukutana na rais wa Marekani Donald Trump Mei 8 2018 katika Ikulu ya Whote House REUTERS/Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Trump amesema wawili hao watakutana na kufanya mazungumzo kupitia barua pepe, kujadili suala hilo  tata ambalo limeharibu uhusiani wa Korea Kaskazini na mataifa mengine ya dunia.

Itakuwa mara ya kwanza, kwa kiongozi wa Marekani kuwasiliana na kiongozi wa Korea Kaskzini katika historia ya hivi karibuni katika ya mataifa hayo mawili.

Ripoti zinasema kuwa Kim Jong Un amekubali kusitisha mradi wa nyuklia na kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu  ili kuzungumza na rais Trump.

Kukutana kwa viongozi hawa wawili, kumetangazwa na mshauri wa masuala ya usalama ya Korea Kusini Chung Eui-yong baada ya kukutana na rais Trump katika Ikulu ya White House.

Chung amesema kiongozi wa Korea Kaskazini yuko tayari kuzungumza naye, na ameomba hilo, ombi ambalo Trump amelikubali.

Wachambuzi wa siasa za Kimataifa wanasema ni mapema sana kuamini iwapo mazungumzo hayo yatafanyika kwa sababu Korea Kaskazini inaweza kubadilisha mawazo wakati wowote.

Shinikizo za rais Trump zinaelezwa kwa kiasi kikubwa kusaidia Korea Kaskazini kuonekana kuja katika meza ya mazungumzo.

Mradi huu wa Korea Kaskazini umeendelea kutishia usalama wa nchi jirani hasa Korea Kusini na kutishia usalama wa Marekani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.