Pata taarifa kuu
URUSI-USALAMA

Putin: Tuna silaha zinazoweza kushambulia popote duniani

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi yake ina silaha mpya za nyuklia ambazo zinaweza kushambulia popote duniani, bila ya kuzuiwa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin asifu jeshi lake na silaha ambazo wanazo kwa sasa.
Rais wa Urusi Vladimir Putin asifu jeshi lake na silaha ambazo wanazo kwa sasa. Sputnik/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya rais Putin imekuja wakati akilihotubia taifa na kuonya kuwa , yeyote atakayetishia usalama wake au wa washirika wake, atashambuliwa vikali.

Wakati wa hotuba yake, mkanda wa video ulionesha silaha hizo zikizrushwa angani, kuonesha uwezo wake wa silaha hizo za nyuklia.

Onyo hili la rais Putin pamoja na onyesho hili, limekuja wakati huu nchi hiyo ikiendelea kuisaidia Syria kupambana na wapinzani wake, wakati huu Damascus ikishtumiwa na watalaam wa umoja wa mataifa kuwa imekuwa ikitumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake.

Marekani imekasirishwa na hatua hiyo na kusema, Urusi kujiviuna kuwa na silaha hizo ni kwenda kinyume cha mkataba wa Kimataifa unaozuia mataifa yenye silaha hizo kuzitumia.

Hata hivyo,wachambuzi wa siasa nchini Urusi wanasema Putin alitumia onyeshi hilo pia kama njia ya kujipatia umaaruifu kuelekea Uchaguizi wa urais tarehe 18 mwezi huu, uchaguzi ambao anatarajiwa kushinda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.