sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Ripoti ya UN yaishtumu Korea Kaskazini kusaidia Syria na silaha za kemikali

media Mashambulizi ya jeshi la serikali ya Syria na mshirika wake Urusi katika eneo la waasi la Ghouta mashariki Februari 27, 2018. REUTERS/ Bassam Khabieh

Gazeti la New York Times nchini Marekani limechapisha ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa, inayodai kuwa Korea Kaskazini imekuwa ikituma silaha za kemikali nchini Syria, zinazotumiwa na wanajeshi wa serikali kuwashambulia wapinzani.

 

 

 

Ripoti hiyo ambayo haijwasilishwa kwa wajumbe wa Umoja wa Mataifa, inaeleza kuwa gesi yenye sumu aina ya Chlorine imekuwa ikitumwa Syria kutekeleza mashambulizi hayo.

Hata hivyo, madai ya Syria kutumia silaha za kemili yamekuwa yakikanushwa na serikali.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, ripoti ya Umoja wa Mataifa imeshtumu Korea Kaskazini kwamba imekuwa ikitumia vifaa Syria ambavyo vinaweza kutumika katika kutengeneza silaha za kemikali.

Vifaa hivyo vinaripotiwa kupatikana kiwizi na kutumwa Syria na Korea Kaskazini vikiwemo vigae venye uwezo wa kuzuia joto na tindi kali nyingi na vipima joto. Vigae vinasemekana kutumika katika kujenga majengo ambapo silaha za kemikali zitatengenezwa.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, ripoti hiyo ambayo haijatolewa rasmi, inasema wataalam wa Korea Kaskazini wameonekana mara kadhaa katika viwanda vya kutengenezea silaha nchini Syria.

Gazeti hilo linasema taasisi ya utafiti ya maswala ya sayansi ya Syria inasemekana kuwalipa Korea Kaskazini kupitia makumpuni bandia.

Serikali ya Korea Kaskazini haijazungumzia lolote kuhusiana na madai hayo, lakini chanzo cha kijeshi nchini Korea Kusini kimesema kuwa kuna uwezekano wa ushirikiano wa kijeshinkati ya Syria na Korea Kaskazini.

Serikali ya Syria imeendelea kushtumiwa kutumia gesi ya klorine katika mashambulizi yake dhidi ya eneo la Ghouta mashariki, linaloshikiliwa na waasi, eneo ambalo linaendelea kuzingirwa na jeshi la serikali.

Shutma hizo dhidi ya Korea Kaskazini zinakuja wakati ambapo nchi hii iinakabiliwa na vikwazo vya kimataifa kufuatia mpango wake wa nyuklia na majaribio ya makombora ya masafa marefu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana