Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Urusi yachunguza sababu ya ajali ya Antonov iliyoua watu 71

media Ndege aina ya Antonov An-148 ya shirika la ndege la Saratov Airlines, ilianguka karibu na mji wa Moscow muda mfupi baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo ( kwenye picha). www.domodedovo.ru

Wachunguzi wa Urusi wanachunguza sababu ya ajali ya ndege aina ya Antonov iliyoanguka karibu na Moscow na kuua watu 71 siku ya Jumapili.

Maafisa hao wa Urusi watachunguza mambo yote ambayo yanaweza kuwa ni sababu ya ajali hiyo ikiwani pamoja na masuala ya hali ya hewa, sababu ya kibinadamu au tatizo la kiufundi - lakini bila kufutilia mbali suala la ugaidi.

Ndege hiyo aina ya Antonov An-148 ya shirika la ndege la Saratov Airlines, ilianguka karibu na mji wa Moscow siku ya Jumapili muda mfupi baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo.

Ndege ilipoteza mawasiliano na mitambo ya uwanja wa ndege, dakika nne baada ya kuondoka kuelekea Orsk, mji wa Urals. Ilianguka katika wilaya ya Ramenski, kilomita 70 kusini mashariki mwa Moscow, karibu na kijiji cha Stepanovskoye.

"Abiria 65 na wafanyakazi sita waliokua katika ndege hiyo, wote walipoteza maisha," ofisi maalumu ya mashita katika masuala ya usafiri ilitangaza katika taarifa yake.

Uchunguzi umefunguliwa rasmi ili kujua uwezekano wa ukiukwaji wa sheria za usalama, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi imetangaza. "

Vladimir Putin ametoa rambi rambi zake kwa familia na kufuta ziara yake iliyokua imepangwa leo Jumatatu katika mji wa Sochi, kusini mwa Urusi

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana