Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-UGAIDI

Watu wenye silaha wavamia kambi ya jeshi jijini Kabul

Watu wenyewe silaha wamevamia kambi ya kijeshi jijini Kabul nchini Afganistan.

Wanjeshi wa Afghanistan katika harakati za kupambana na ugaidi
Wanjeshi wa Afghanistan katika harakati za kupambana na ugaidi reuters
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Ulinzi Dawlat Waziri amesema wanajeshi watano wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika makabialiano.

Kundi la Islamic State limedai kutekeleza shambulizi hilo kupitia jarida lake la propaganda  linalofahamika kama Amaq.

Walioshuhudia uvamizi huo wamesema  walisikia milipuko ya risasi hewani  katika kambi hiyo na kufuatiwa na makabiliano makali.

Mwezi Oktoba mwaka uliopita, kundi la Taliban lilivamia kambi ya kutoa mafunzo kwa wanajeshi na kusababisha vifo vya wanajeshi 15 kupoteza maisha.

Mbali na uvamizi katika kambi za jeshi, mwishoni mwa wiki iliyopita, zaidi ya watu 100 waliuawa baada ya gaidi wa Taliban kujilipua katika eneo ambalo lilikuwa na watu wengi.

Hali kama hiyo ilishuhudiwa hivi karibuni baada ya wapiganaji hao kuvamia hoteli ya kifahari ya Intercontinental jijini Kabul na kusababisha vifo vya watu 25.

Serikali ya Afghanistan, imeshindwa kushinda ugaidi nchini humo kwa muda mrefu sasa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.