Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Afghanistan yaomboleza vifo vya zaidi ya watu 100 jijini Kabul

media Gari la wagonjwa lilotumiwa kutekeleza shambulizi la bomu jijini Kabul nchini Afghanistan REUTERS/Omar Sobhani

Watu zaidi ya 100 wamethibitishwa kupoteza maisha jijini Kabul nchini Afganistan baada ya mlipuko wa bomu ndani ya gari la kubeba wagonjwa siku ya Jumamosi.

Serikali ya Afganistan imetangaza siku tatu za maombolezo na kulaani shambulizi hilo la kigaidi.

Kundi la Taliban limekiri kutekeleza shambulizi hilo baya jijini Kabul katika siku za hivi karibuni.

Ripoti zinasema kuwa, walipuaji waliendesha gari hilo la wagojwa kulipokuwa mkusanyiko wa watu na kujilipua.

Waziri wa Mambo ya ndani Wais Barmak amesema watu wengi walipoteza maisha wakati wakipata matibabu hospitalini na watu wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa, hasa wanaume.

Shambulizi hili limezua hali ya wasiwasi jijini Kabul, na kusababisha watu wengi kuamua kusalia majumbani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana