Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
Asia

Moto waua watu zaidi ya 41 katika hospitali Korea Kusini

media Moto wazuka katika hospitali ya mji mdogo wa Miryang kusini-mashariki mwa nchi umesababisha maafa mengi. Yonhap/Reuters

Moto mkubwa uliozuka leo Ijumaa katika hospitali moja nchini Korea Kusini, umeua watu wasiopungua 41 kwa mujibu wa shirika la habari la Yonhap, maafa mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja.

Watu zaidi ya 80 wamejeruhiwa pia katika janga hili linalotokea wiki moja kabla ya kuwasli nchini humo maelfu ya wanariadha na wageni kwa mashindano ya Olimpiki ya Majira ya baridi.

Katika video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya wagonjwa waliokolewa na helikopta kwa kutumia kamba juu ya hospitali ya Miryang kusini-mashariki mwa Korea Kusini. Na wengine wamekua wakiokolewa kwa kupitishwa kwenye madirisha mbalimbali.

Moto umezuka katika hospitali ya Miryang, Kusini-Mashariki mwa Korea Kusini: wagonjwa waokolewa. Kim Dong-min/Yonhap via REUTERS

Jengo hilo la ghorofa sita lina sehemu wanakohudumia wazee pamoja na sehemu ya hospitali.

Idadi ya vifo imeenelea kupanda toka asubuhi wakati ambapo waliojeruhiwa wameendelea kupoteza maisha kutokana na kukosa hewa baada ya jengo hilo kuendelea kuteketea kwa moto. Mapema idadi ya waliopoteza maisha ilikua imefikia 41, kwa mujibu wa shirika la habari la Yonhap, ambalo limenukuu maafisa wa Zima Moto waliopo kwenye eneo la tukio.

"Wauguzi wawili wamesema kwamba waliona moto ghafla katika chumba cha huduma ya dharura," amesema Mkuu wa Zima Moto, Choi Man-Woo.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana mpaka sasa.

Wagonjwa wote waliondolewa, ameongeza, huku akibaini kwamba waathirika wote walikuwa katika hospitali.

"Wengi wa waathirika walikuwa kwenye ghorofa ya kwanza na ya pili ya hospitali (...)." Baadhi wallifariki dunia wakati wakipelekwa hospitali nyingine.

Watu wapatao 200 walikuwa katika jengo hilo ambako kunapatikana hospitali ya Sejong wakati moto ulizuka, polisi wamesema.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In alielezea masikitiko yake katika mkutano wa dharura na washauri wake, mkutano ambao ulikua na lengo la kuamua hatua ambayo inaweza kuchukuliwa,kwa mujibu wa msemaji wake.

Alitoa wito kwa wachunguzi kutoa haraka sababu za janga hilo ili "kuepuka hali ya sintofahamu kwa familia," amesema Park Soo-Hyun.

Tukio hili linatokea mwezi mmoja baada ya moto kuzuka kwenye klabu ya michezo ya kunyoosha misuli katika mji wa Jecheon, ambapo watu 29 walipoteza maisha.

Janga hili ni baya zaidi kuwahi kutokea nchini Korea Kusini kwa zaidi ya muongo mmoja. Mnamo mwaka 2003, moto ulizuka kwenye kituo cha treni za mwendo kasi katika mji wa Daegu, kusini-mashariki mwa Korea Kaskazini, tukio lililosababisha vifo vya watu 192 na karibu 150 walijeruhiwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana