Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini yanaendelea

media Wajumbe kutoka Korea ya Kaskazini na Kusini, Januari 15, 2018 katika kijiji kilio mpakani cha Panmunjom (upande wa kaskazini), wakati wa mazungumzo kuhusu kushiriki kwa wanamichezo wa Korea Kaskazini Mashindano ya Olimpiki ya Pyeongchang. The Unification Ministry/Yonhap via REUTERS

Wajumbe wa Korea Kaskazini na Kusini wameanza mazungumzo kuhusu namna wanamichezo wa Korea Kaskazini watakavyoshiriki katika michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi mwezi ujao.

Mataifa hayo mawili wiki iliyopita, yalikubaliana kutuma wachezaji wa Korea Kaskazini watakaoshiriki katika michezo hiyo, hatua ambayo itasaidia kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Korea Kusini imekuwa ikitaka mazungumzo zaidi ikiwemo masuala ya usalama, lakini Korea Kaskazini imetaka mazungumzo hayo kuzingatia ushiriki wa wachezaji wake kuhusu michezo ya Olimpiki.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika eneo la Panmunjom, katika mpaka wa nchi hizo mbili, eneo ambalo linaelezwa la kihistoria kati ya nchi hizo mbili.

Mazungumzo ya mwisho kati ya nchi hizi mbili, yalifanyika mwaka 2015. Haijafahamika ni nani watakaohudhuria mazungumzo haya mapya.

Hatua hii, imeonekana kutuliza uhasama kati ya nchi hizi mbili, kutokana na mradi wa Korea Kaskazini kuzalisha silaha za nyuklia.

Korea Kaskazini imekuwa ikitishia kuishambulia Marekani na washirika wake kama Korea Kusini.

Rais wa Marekani Donald Trump amepongeza hatua hiyo ya kuwepo kwa mazungumzo hayo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana