Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Asia

Korea Kaskazini na Korea Kusini zakutana kwa mazungumzo

media Katika mji wa Seoul, raia wa Korea Kusini wanafuatilia kwa karibu kwenye televisheni taarifa kuhusu mazungumzo kati ya Korea kaskazini na Korea Kusini katika kijiji cha PanmunjomJumanne, Januari 9, 2018. REUTERS/Kim Hong-Ji

Korea Kaskazini na Korea Kusini zimeanza mazungumzo ya kihistoria baada miaka 2 ya uhasama. Mazungumzo haya yanafanyika katika kijiji cha Panmunjom kuhusu uwezekano wa Korea Kaskazini kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi yatakayofanyika Korea Kusini mwezi wa pili.

Uhusiano kati ya nchi hizi mbili ulidorora baada ya Korea Kusini kukatisha mradi wa pamoja wa kiuchumi katika eneo la kiuchumi la Kaesong nchini Korea Kaskazini, na kufuatiwa na majaribio ya nyuklia yaliofanywa na Korea Kaskazini.

Kijiji hicho hujulikana kama kijiji cha pande mbli, ambapo kila upande una miliki sehemu yake na katikati kuna jengo la umoja wa mataifa. Baada ya vita ya korea kuisha mwaka 1953 kijiji cha Panmunjom kiliamuriwa kuwa sehemu ya pande zote mbili, na maofisa wa pande zote mbili wanatarajiwa kukutana katika kijiji hiki.

Mazungumzo ya mwisho baina ya nchi hizo mbili yalifanyika Disemba mwaka 2015 nchini Korea ya Kusini.

Waziri wa Muungano wa Korea Kusini , Cho Myoung-Gyon amesema mazungumzo hayo yanajikita zaidi katika masuala ya olimpiki lakini mambo mengine pia yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili hasimu.

Waziri Cho Myoung-Gyon ambaye ataongoza mazungumzo hayo amesema serikali yake itazungumzia pia suala la matokeo ya vita na njia za kupunguza mvutano wa kijeshi.

Korea Kaskazini imewakilishwa katika maungumzo hayo na maafisa watano wakiongozwa na Ri Son-gwon ambaye ni mwenyekiti wa Idara ya serikali ya Korea ya Kaskazini mwenye dhamana ya masuala na Kusini.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana