Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Watu tisa wauawa Isfahan, Iran

Watu tisa waliuawa usiku wa Jumatatu kuamkia leo Jumanne wakati wa maandamano ya kuipinga serikali katika jimbo la Isfahan katikati mwa Iran, televisheni ya serikali imeripoti leo Jumanne

Kiongozi Mkuu Ali Khamenei mnamo Januari 2, 2018 amewashtumu "maadui wa Iran kuchochea maandamano yanayoibuka nchini Iran kutoka nchi kadhaa.
Kiongozi Mkuu Ali Khamenei mnamo Januari 2, 2018 amewashtumu "maadui wa Iran kuchochea maandamano yanayoibuka nchini Iran kutoka nchi kadhaa. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa televisheni ya serikali, watu sita waliuawa katika mji wa Qahderijan, mwingine aliuawa katika eneo la Khomeini Shah, na mpiganaji mmoja wa kundi la wanamgambo la Bassidji na polisi mmoja waliuawa katika eneo la Najaf Abad.

Kwa jumla, zaidi ya watu 21 wameuawa tangu kuanza kwa maandamano hayo tarehe 28 Desemba 2017 , kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.Siku ya Jumatatu, Januari 1, 2018, afisa wa polisi aliuawa wakati wa vurugu zinazohusiana na maandamano ya kuipinga serikali.

Nyimbo dhidi ya serikali zinaendelea kusikika katika mitaa ya Tehran. Jumatatu jioni Januari 1, 2018, uwepo wa polisi katika mitaa mbalimbali haujabadilisha chochote. Makundi kadhaa ya waandamanaji yameendelea kukusanyika katikati ya mji mkuu, Tehran.

Mamlaka imeanza kushambulia viongozi wa maandamano hayo. Polisi imewakamata watu kadhaa. Video zilizorushwa kwenye mitandao ya vyombo vya habari vya Iran na mitandao ya kijamii zimethibitisha matukio hayo.

Rais wa Iran Hassan Rouhani amelaani vurugu zinazoendelea na saa chache baada ya polisi mmoja kuuawa katika mji wa Najafabad, katika mwa nchi. Rais Rouhani amesema serikali yake imeamua "kutatua matatizo ya wananchi," hasa ukosefu wa ajira.

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump amewapongeza waandamanaji nchini Iran akisema kuwa wanapaswa kuungwa mkono. Rais Rouhani amemwita rais wa Marekani adui wa taifa lake, ambaye lengo lake ni kuchochea vurugu kwa minajili ya kuuangusha utawala uliopo.

Hayo yakijiri jeshi la mapinduzi nchini humo limeonya kuwa litatumia nguvu dhidi ya waaandamanaji wa upinzani wanaoendelea kujitokeza katika miji mbalimbali.

Mkuu wa jeshi hilo ameonya kuwa, waandamanaji sasa wameanza kuimba nyimbo za kisiasa wakichoma moto mali ya umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.