Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Trump aishtumu China kuendelea kutoa mafuta kwa Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kuishtumu China kwamba inaendelea na mpango wake wa kutoa mafuta kwa Korea Kaskazini na kuongeza kuwa hatua hiyo inaweza kuzuia kupata "suluhisho la kutosha" katika mgogoro unaosababishwa na majaribio ya makombora ya masafa marefu ya korea Kaskazini.

Rais wa Marekani ailaumu China kwa kutoa mafuta kwa Korea Kaskazini.
Rais wa Marekani ailaumu China kwa kutoa mafuta kwa Korea Kaskazini. REUTERS/Kevin Lamarque/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii, inakwenda kinyume na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataufa ambalo liliiwekea vikwazo, Korea Kaskazini kununua mafuta nje ya nchi hiyo kwa lengo la kuizua kuendelea na maradi wake wa nyuklia.

Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema inavyoonekana haiwezekani kukawa na mwafaka wa kirafiki kuhusu Korea Kaskazini.

"Ninaskitishwa sana kuona China inaendelea kutoa mafuta kwa Korea Kaskazini. Kamwe hakutakua na suluhisho kwa tatizo la Korea Kaskazini ikiwa hatua hiyo haitasitishwa mara mojai! " aliandika Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mapema siku ya Alhamisi China ilisema kuwa hakujakua na usafirishaji wowote wa mafuta kwa meli kwenda Korea Kaskazini kinyume na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Gazeti la Korea Kusini limeripoti kwamba meli za China na Korea Kaskazini zilikutana katika bahari kinyume cha sheria kwa kusafirisha mafuta kuelekea Korea Kaskazini.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, serikali ya Marekani ilipewa taarifa kuhusu bidhaa mafuta na makaa ya mawe ambavyo vilisafirishwa kuelekea Korea Kaskazini.

"Tuna ushahidi kwamba meli zilizoohusika katika shughuli hiyo zinamilikiwa na makampuni kutoka nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na China," alisema afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Katika mahojiano na gazeti la New York Times, Donald Trump amesema alikuwa mpole kwa China, hasa juu ya suala la biashara, huku akibaini kwamba amesikitishwa kuona China inatoa mafuta kwa Pyongyang.

"Nimekuwa mpole kwa China, kwa sababu kwa mtazamo wanguu kitu pekee ambacho ni muhimu zaidi kuliko biashara ni vita," Donald Trump amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.