Pata taarifa kuu
CAMBODIA-SIASA-HAKI

Cambodia yakabiliwa na vikwazo baada ya kufuta upinzani

Marekani imesema itachukua "hatua kali" dhidi ya Cambodia, na Umoja wa Ulaya umeatishia kuweka hatarini mpango wa biashara ambao unanufaisha nchi hiyo, baada ya chama kikuu cha upinzani kupigwa marufuku kushiriki uchaguzi.

Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Sen, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa Ufaransa, Novemba 9, 2017.
Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Sen, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa Ufaransa, Novemba 9, 2017. REUTERS/Samrang Pring
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi Mahakama Kuu ya Cambodia alifuta chama kikuu cha upinzani CNRP, kwa ombi la Waziri Mkuu Hun Sen, ambaye anataka kusalia mamlakani bila upinzani. Hun Sen yuko madarakani kwa zaidi ya miaka 30.

Kiongozi wa CNRP Kem Sokha alikamatwa tarehe 3 Septemba akishtumiwa kujaribu kupindua serikali ya zamani ya Khmer Rouge kwa ushirikiano na Marekani.

Wakosoaji wa Hun Sen wameelezea hatua hiyo ya kufuta chama cha upinzani kuwa ni jaribio la wizi wa kura, wakiongeza kwamba ulikua wakati mzuri wa kuimarisha demokrasia baada ya wafadhili wa Magharibi kutoa mabilioni ya dola kuanzia mwaka 1993 ili kuanzisha mfumo wa vyama vingi baada ya miongo kadhaa ya vita.

"Ikiwa mambo yanakwenda kwa hali ilivyo sasa, uchaguzi wa mwaka ujao hautakuwa wa halali na wa haki," ikulu ya White House imesem akatika taarifa yake.

Miongoni mwa hatua za kwanza zilizotangazwa, Marekani itasitisha kutoa fedha kwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini Cambodia.

Mjini Brussels, msemaji wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa uchaguzi utakua umepoteza uhalali wote kama upinzani hautashiriki, akibainisha kuwa heshima kwa haki za binadamu ni sharti ya kunufaika kwa mpango wa biashara wa Umoja wa Ulaya.

Serikali ya Phnom Penh haijajibu kuhusu vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya na Marekani.

Mahakama pia ilipiga marufuku wanasiasa 118 wa upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa kipindi cha miaka mitano.

Binti yake, Kem Monovithya, ambaye pia ni mwanasiasa wa chama cha CNRP, amesema kuwa uamuzi huo wa mahakama haujawashangaza.

Wafadhili wa Cambodia wameomba kuachiliwa kwa Kem Sokha lakini wanaonekana kusita kuweka vikwazo dhidi ya nchi ambayo ni mshirika wa karibu wa China.

Hun Sen, katika taarifa yake iliyorushwa kwenye televisheni na kwenye Facebook, amehakikisha kwamba uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Julai mwaka ujao "utafanyika kama ilivyopangwa."

Wanasiasa wa chama cha CNRP ambao hawajapigwa marufuku kufanya shughuli yoyote ya kisiasa wana haki ya kuunda chama kipya, amesema Hun sen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.