Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-UN-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini: Siwezi kufanya mazungumzo mpaka Marekani ijirekebishe kwa kauli zake

Korea Kaskazini imeuambia Umoja wa Mataifa kuwa nchi hiyo haina mpango wa kufanya mazungumzo na nchi yoyote kuhusu mipango yake ya nyuklia mpaka Marekani itakapobadili sera yake ya uadui.

Kiongozi wa Korea Kaskazini ameendelea kuionya Marekani kutoendelea kuitishia kuishambulia kijeshi.
Kiongozi wa Korea Kaskazini ameendelea kuionya Marekani kutoendelea kuitishia kuishambulia kijeshi. KCNA via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Naibu Balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa Kim In Ryong ameiambia kamati maalumu ya silaha ya Umoja wa mataifa kuwa hali ya mambo kwenye rasi ya Korea ni mbaya na inaweza kuibua vita vya nyuklia.

Korea Kaskanini imetekeleza majaribio ya makombora ya masafa marefu kama sehemu ya mpango wake wa nyuklia katika rasi ya Korea na kuibua mvutano baina yake na jumuiya ya kimataifa.

Hivi Karibuni Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi w a Pyongyang Kim Jong Un waliingia katika mvutano wa maneno baada ya Trump kutishia kuisambaratisha Korea Kaskazini ikiwa itaendelea kutekeleza mipango yake ya nyuklia.

Hata hivyo waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Rex Tillerson amenukuliwa na kituo cha CNN akisema rais Trump ana mpango wa kuepusha vita dhidi ya Korea Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.