Pata taarifa kuu
BURMA-USALAMA

Watu wengi kutoka jamii ya Rohinga wamekufa maji

Takriban watu 12 wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani waliko baada boti lililokua likisafirisha wakimbizi kutoka jamii ya Waislamu wa Rohingya waliokua wakikimbia kutoka Burma.

Wakimbizi wa Rohingya wkiwasili Bangladesh wapelekwa katika kambi ya Bazar ya Cox, tarehe 2 Oktoba 2017.
Wakimbizi wa Rohingya wkiwasili Bangladesh wapelekwa katika kambi ya Bazar ya Cox, tarehe 2 Oktoba 2017. REUTERS/Cathal McNaughton
Matangazo ya kibiashara

Hili ni janga jipya kufuatia ukiukwaji wa haki za binadamu uliosababisha nusu milioni ya watu kutika jamii ya Rohinya kukimbilia nchini Bangladesh katika kipindi cha wiki sita .

"Mawimbi yalikua mengi ten amakubwa, tunadhani kwamba wamepoteza udhibiti wa boti lao," amesema Rony Mitra, afisa wa zim amoto ambaye anapiga doria na wenzake kwenye pwani ya Shah Por Dwip, katika zoezi la kutafuta miili ya watu walipotez amaisha, kwa ujibu wa shirika la Habari la AFP.

Ajali hii ilitokea siku yaJumapili usiku katika Bahari ya Bengal, karibu na Mto Naf, unaotenganisha Burma na Bangladesh.

Rohingyas wanakabiliwa hali nzito kwa wiki kadhaa, wakitoroka machafuko yanayowalenga, machafuko yanayotekelezwa na jeshi la Burma, baada ya mashambulizi ya waasi wa Rohingwa karibu na mipaka ya nchi hiyo.

Kwa wakati huo, waokoaji hawajui ni watu wangapi waliokuwa kwenye boti hiyo. Inaripotiwa kuwa watu walio kati ya 60 na 100 huenda walikua katika boti hilo, kulingana na ushuhuda wa manusura, ambao wamethibitisha kwamba watoto wengi walikua katika boti hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.