Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini yailaumu Marekani kwa kutangaza vita

Serikali ya Korea Kaskazini kupitia Waziri wake wa Mambo ya Kigeni imesema kwamba rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vita dhidi ya Korea Kaskazini. Vita vya maneno kati ya nchi hizi mbili zinaendelea, huku kila upande ukilaumu kuhatarisha usalama wa mwengine.

Viongozi wa Korea ya Kaskazini kwenye kituo cha silaha za nyuklia.
Viongozi wa Korea ya Kaskazini kwenye kituo cha silaha za nyuklia. KCNA via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kora Kaskazini, Ri Yong-ho, aliwaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini ina haki ya kudungua ndege za vita za Marekani, na “ni katika hali ya kujihami”.

Bw Yong-ho amesema watafanya hivo hata kwa zile ndege zenye hazipo katika anga ya Korea Kaskazini.

Bw Yong-ho amesema kuwa Marekani ndioo ilikuwa ya kwanza kutangaza vita dhidi ya Korea Kaskazini..

Pande hizo mbili zimekuwa zikitupiana maneno makali.

Kifaa cha hivi karibuni kilichorushwa na Korea ya Kaskazini kilipitia katika anga ya Japan tarehe 29 Agosti.
Kifaa cha hivi karibuni kilichorushwa na Korea ya Kaskazini kilipitia katika anga ya Japan tarehe 29 Agosti. REUTERS/Kim Kyung-Hoon/File Photo

Katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa hivi karibuni Donald Trump alisema kuwa ataisambaratisha Korea Kaskazini. Siku chache baadae kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alimtusi Donald Trump kuwa ni mtu mwenye ugonjwa wa akili.

Hivi karibuni rais Donald Trump kupitia mtandao wa twitter, aliandika kuwa Bw. Yong-ho na Kim Jong-un hawataendelea kuwepo kwa muda ikiwa wataendelea na maneno yao ya kejeli na vitisho.

Vita hivi vya maneno kati ya nchini hixi mbili hasimu vilianza baada ya Korea Kaskazini kupuuzia onyo na vikwazo vya Marekani na Umoja wa Mataifa na kuendelea na mpango wake wa nyuklia pamoja na kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Ri Yong-ho, katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 23, 2017.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Ri Yong-ho, katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 23, 2017. REUTERS/Eduardo Munoz

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.